
Vijana wengi wamekuwa wakiwekeza katika sekta ya uandishi wa habari na utangazaji hapa nchini. Kaka yenu nimejitahidi kumtafuta kijana mmoja ambaye nimeweza kuongea naye mawili matatu.
Kaka Yako: Habari yako braza?
G-Voice: Safi kaka
Kaka Yenu: Ningefurahi kama ungetutajia jina lako halisi.
G-Voice:Mimi naitwa Grey gory Henry. a.k.a G-voice a.k.a Mo fire.
Kaka Yenu: Niambie Unafikiri ni kwa nini vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika fani hii ya utangazaji kwa kasi kubwa
G-Voice: Mimi nafikiri sababu kubwa ni kwamba kwanza kazi hii ya utangazaji ni rahisi hata kwa kuisomea kwani kozi zake ni fupi fupi, na pili inawatazama zaidi vijana tofauti na hapo zamani.
Kaka Yenu : Wewe kwa upande wako ni mtangazaji gani aliyekuvutia na kukufanya uipende kazi hii?
G-Voice: kwa kweli mimi namzimia sana Fredwaa pamoja na Deo Kaji Makomba
Kaka Yenu: Kwa nini.
G- Voice: The way wanavyo present
Pichani juu G-Voice akiwajibika studioni katik kipindi chake
cha triple deka. ' kweli mnyamwenga ni mo fire'
Pamoja na hayo yote lakini mshikaji na mshabiki mkubwa wa Mopao Mokonzi 'Koffi Olomide'
Nilipomuuliza kuhusu changamoto yake kwa vijana amesema vijana wasibweteke kwani maisha ni magumu hivyo hakuna budi kujituma kwa bidii zote.
Jamaa kwa sasa anachapa mzigo katika radio maarufu kule katika visiwa vya Zanzibar inayoitwa CHUCHU FM.
Kuhusu suala la familia ameniambia kwa sasa bado yupo yupo kwanza ila ana mchumba ambaye anamzimia kinoma.
Kaka Yenu: ahsante sana braza kwa taim yako.
G-Voice: ahsante.
Ukitaka kuujua ukali wa mchizi ahuyo hapo!!!! mnyamwenga huyo hapo!!!! tegea sikio chuchu fm kila siku ya j'3 hadi alhamis kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku.
Blog hii inamtakia kila la heri G-Voice.