NABIL ABIL AL- FADL
MBUNGE wa
Kuwait Nabil al-Fadl (65) amefariki dunia ghafla leo baada ya kuanguka
kutoka kwenye kiti chake bungeni wakati wa kikao cha bunge la nchi hiyo.

BUNGE LA KUWAIT
Wabunge
walimzingira na kutaharuki hali iliyojitokeza bungeni humo wakati Waziri
wa Afya wan chi hiyo, Dkt Ali al-Obaidi akijaribu kumtibu hadi wakati
madaktari walipowasili.
Marehemu
Al-Fadl — ambaye alikuwa ni mwandishi wa habari alikuwa maarufu kwa
kutumia jarida lake kuwaasa wabunge wenzake na hata wakati mwingine
kuwakosoa.
Aidha Al-Fadl alifahamika zaidi kwa kuwakaripia waasi wa Kiislamu ambao aliwashambulia kwa maneno makali.
Wakati mmoja aliwashangaza wasomaji wake alipoitaka serikali iondoe mara moja marufuku ya uuzaji wa pombe na maeneo ya burudani.