MAREHEMU ADAM KUAMBIANA
Siku chache
baada ya kifo cha mwongozaji na muigizaji wa kiwanda cha filamu za Bongo, Adam Philip
Kuambiana, daktari mkubwa wa mastaa hao ameibuka na kudai marehemu alijiua
mwenyewe.
Kwa mujibu
wa daktari huyo ambaye hakupenda jina lake lipate nafasi katika blog hii kutokana na
maadili ya taaluma yao kuficha siri ya mgonjwa, ametonya kwamba siku moja kabla ya kifo
(Ijumaa ya Mei 16, mwaka huu), marehemu alimpigia simu na kumwambia
amekunywa dawa za malaria aina ya Fansidar lakini pia amekunywa pombe.
Daktari
huyo alieleza kuwa, marehemu alimpigia simu kumuomba ushauri juu ya
nini cha kufanya na kama kuna madhara yoyote juu ya pombe hizo na dawa
alizokunywa.
“Aliniuliza
kama kuna madhara yoyote ambayo anaweza kuyapata kwa kuwa alikuwa
amekunywa fansidar kwa ajili ya malaria kisha akapata kiu ya bia na
kuamua kunywa,” alisema daktari huyo.
Akizidi
kuzungumzia tukio hilo, Daktari amesema licha ya
msanii huyo kuwa na ‘masihara’ mara kwa mara, lakini kwa kuwa
alimwambia jambo ambalo linahusu uhai wake, alimshauri kwenda hospitali
iliyo karibu ili akaonane na daktari kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa
kutoa sumu kwani kitaalam mtu anapokunywa pombe akiwa amemeza dawa za
aina hiyo vyote hugeuka kuwa sumu.
MWENYEZI MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU ADAM PHILIP KUAMBIANA.