CECAFA YAJICHANGANYA, YAIBADILISHIA MBEYA CITY RATIBA, TIMU ZOTE ZA
MISRI ZAGOMA MBEYA CITY YAKWEA PIPA USIKU HUU.
BARAZA la
Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limesogeza mbele kwa siku
mbili michuano yake mipya ijulikanayo kama Nile Basin na sasa itaanza kesho
wakati wawakilishi wa Tanzania, Mbeya City wataondoka usiku wa leo kwenda
Sudan.
Taarifa
ya CECAFA iliyotumwa leo imesema kwamba timu zote za Misri zilizotarajiwa
kushirki michuano hiyo hazitakuja tena na baadhi ya timu zilizowekwa kwenye
ratiba awali zimejitoa na nafasi yake kupewa timu nyingine.
Sasa
michuano hiyo inayoshirikisha mabingwa wa Kombe la Fa na washindi wa pili wa
Ligi Kuu za nchi wanachama wa CECAFA makundi yake matatu yamepangwa upya pamoja
na ratiba nzima.
Kundi A sasa
litakuwa na timu za El Merreikh ya Sudan, Victory University ya Uganda, Malakia
ya Sudan Kusini na Polisi ya Zanzibar, Kundi B kuna Mbeya City ya Tanzania
Bara, AFC Leopars ya Kenya, Academie Tchite ya Burundi na Entincelles ya
Rwanda, wakati Kundi C kuna Al Shandy ya Sudan, Defence ya Ethiopia na Dkhil ya
Djibouti.
Awali
michuano hiyo ilitarajiwa kushirikisha timu za Misri pia, Al Masry, Hey Al
Arab, Arab Contractors, zilizoalikwa kunogesha mashindano hayo, lakini
zikajitoa dakika za mwishoni.
Kwa ujumla,
awali timu zilizotarajiwa kushiriki mashindano hayo ni Al Ahly Shandy, Al Masry
ya Misri, Defence na Dhikil zilizopangwa Kundi C, wakati Kundi D lilikuwa na
Hey Al Arab, Arab Contractors, Flam beaude L'EsT ya Burundi na Etincelles ya
jijini Kigali, Rwanda.
Mbeya
City imeendelea kubaki Kundi B kama ilivyo AFC Leopard ya Kenya, lakini El
Mereikh Al Fashery na Elman ya Somalia zimeondoka na nafasi yake
imechukuliwa na Enticelles na Academie Tchite.
Mbeya
City sasa itatupa karata yake ya kwanza Jumamosi mbele ya Academie Tchite ya
Burundi Uwanja wa Merreikh kuanzia Saa 11:30 jioni na kufuatiwa na mchezo kati
ya AFC Leopards ya Kenya na Enticelles ya Rwanda Saa 2:00 usiku, hizo zikiwa
mechi za Kundi B.
Mechi
tatu za Ufunguzi zinatarajiwa kuchezwa kesho, kati ya Victoria Univesrity ya
Uganda na Malakia ya Sudan Kusini, wenyeji Al-Merreikh ya Polisi ya Zanzibar
zote zikiwa za Kundi A na wenyeji wengine Al-Shandy dhidi ya Dkhill ya
Djibouti, huo ukiwa mcheo wa Kundi C.
Katibu
Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, ameithibitisha kupatiwa tiketi na leo usiku
wanapanda ndege kwenda Sudan.
SALEH NA JULIO WAITIA HALUA MCHANGA MSIMBAZI.
Kazi imeanza,
mapingamizi yameanza ndani ya klabu ya Simba na moja ni lile alilowekewa
mgombea wa Urais wa Simba, Michael Wambura.
Wambura amewekewa
pingamizi na Saleh Majaba wa Arusha ambaye anasema alifanya kampeni kabla ya
uchaguzi.
Majaba ambaye ni
mwanachama wa Simba kutoka Arusha amesema Wambura alianza kampeni kabla ya
uchaguzi, kitu ambacho si sahihi.
Upande mwingine,
Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye ni mgombea wa nafasi ya makamu wa rais
amewawekea pingamizi wagombea wote wanaotokea kwenye kamati ya utendaji.
Julio amewapinga
Swed Nkwabi ambaye anagombea naye nafasi moja, Ibrahim Masoud Damian Manembe na
Said Pamba.
SUAREZ OUT KOMBE LA DUNIA
Mshambuliaji
Luis Suarez wa Liverpool ameumia mazoezini na ataikosa michuano ya Kombe la
dunia inayonza mwezi ujao nchini Brazil.
Suarez ameumia goti wakati wa
mazoezi ya timu yake ya taifa ya Colombia na atatakiwa kuwa nje ya uwanja
kuanzia wiki nne hadi sita.
Mwenyewe ameonekana kuwa na
majonzi lakini hana ujanja kuwa ataikosa michuano hiyo.
Waingereza wameonekana kufurahia
huku mashabiki wengi wakionyesha furaha hiyo kwenye mitandao ya kijamii kama
Twitter, Facebook na Instagram.
England ilikuwa inakipiga na
Uruguay Juni 19 na mashabiki wake wanajua shughuli ya mbaguzi huyo ambaye ndiye
mchezaji bora wa Ligi Kuu England .
MAKELELE APATA ULAJI UFARANSA, SASA KOCHA
MKUU LIGUE 1
KIUNGO wa
zamani wa Chelsea, Claude Makelele ataachia nafasi yake ya Ukoha Msaidizi wa
PSG ili aka we kocha mpya Mkuu wa timu ya Ligue 1 pia, Bastia.
Makelele,
ambaye enzi zake alichezea klabu za Real Madrid, Chelsea na PSG anaweza
kutambulishwa kama kocha mpya wa Bastia kabla ya mwishoni mea wiki kwa
mujibu wa gazeti la Ufaransa, L'Equipe.
PSG
ilimpa Makelele ofa ya Mkataba wa miaka miwili zaidi, lakini amegoma
ili aka we bosi kamili timu nyingine.
Ataungana
na mchezaji mwenzake wa zamani wa Ufaransa, Willy Sagnol kuwa kocha mpya Mkuu
katika Ligue 1 baada ya beki huyo wa zamani wa Bayern Munich kuwa mbioni
kuteuliwa kocha mpya wa Bordeaux.
Makelele,
mwenye umri wa miaka 41, alikuwa chachu ya mafanikio ya mwanzoni ya kocha Mreno
Jose Mourinho Stamford Bridge.
Akiwa
amesajiliwa kutoka Real Madrid mwaka 2003, Makelele alikuwa mchezaji muhimu mno
katika mfumo wa Mourinho wa 4-3-3, akiwafanya watu Frank Lampard kufunga sana
mabao.
MAN UNITED YAANZA RASMI USAJILI, YAKUBALI KUMNUNUA KIUNGO WA BAYERN
MUNICH
KLABU ya
Manchester United imekubakli kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos na
sasa inaelekeza nguvu zake kwa mchezaji mwenzake Arjen Robben.
day la
Pauni Milioni 20 kumnunua Kroos lilikubaliwa wakati David Moyes bado yupo
kazini Old Trafford na mroithi wake kocha wa zamani wa Bayern, Louis van
Gaal, imeelezwa ameruhusu mango uendelee.
Kroos,
mwenye umri wa miaka 24, alifundishwa na Van Gaal alipokuwa Bayern na yuko
tayati kufanya kazi tena na kocha wake wa zamani.
SAGNA SASA
KUHUDUMU MAN CITY MSIMU UJAO KWA MSHAHARA WA PAUNDI 150,000 KWA WIKI.
Kocha Manuel Pellegrini ameshinda
vita ya kumpata full back kutoka Arsenal, Bacary Sagna.
Sagna amekubali kusaini mkataba
wa miaka mitatu baada ya kuahidiwa mkataba ambao atakuwa analipwa pauni 150,000
kwa wiki.
Beki huyo Mfaransa amesafiri
kwenda jijini Manchester na taarifa zinaeleza tayari Sagna amefuzu hadi vipimo na
kilichobaki ni kusaini baada ya muda mchache ujao.