
Japo kuwa alikuwa na mwili mkubwa ambao ulimfanya aitwe (jitu la miraba kumi na mbili) lakini alikuwa na uwezo mkubwa katika kulishambulia jukwaa katika miondoko ya soukouss.Anaitwa Joseph Kabasele Yampanya a.k.a pepe kale, Ambaye alikuwa ni mmiliki ama Prezidaa wa bendi L' Empire Bakuba ni mmoja kati ya wanamuziki waliofanya vizuri sana katika tasnia ya muziki hasa muziki huu wa kiafrika kutokea kule kinshasa kati kati ya jiji la Congo, kama hio haitoshi Pepe amekuwa akipata heshima sana tu kutoka kwa wanamuziki mbalimbali wakiwemo Djuna Mumbafu, Dilu Dilumona, Dominique Mabwa, Germain Kanza pamoja na Lofombo ambaye ndiye anasadikika alikuwa ni mtu wa karibu sana wa Pepe Kale.Na pengine kama yanayosemwa ni kweli basi amini kwamba mtoto wa nyoka ni nyoka, namaanisha ndani ya kundi la Akudo Impact linaloongozwa na Christian Bella inasemekana Allain Kabasele ni mtoto wa nguli huyo wa soukouss (PEPE KALE).

Huyu pia na yeye ni mkongwe ktk burudani kutokea kule nchini Congo anaitwa Koffi Charles Antoinne Olomide 'mopao mokonzi' na yeye ni mmoja kati ya waliokuwa wakizikubali kazi za pepe kalle. Haya mdau kazi kwako, mimi natia nanga hapa. Wenyewe wanakwambia,
NABANZIO YOKI.!!!!