Wakati Tasnia ya filamu Bongo ikiwa katika majonzi ya kuondokewa na ‘dairekta’
na mwigizaji mkubwa, Adam Phillip Kuambiana (38), pigo lingine
limetokea kwa wasanii hao kwa kuondokewa na kichwa kingine, Sheila Haule
‘Recho’ (26). Recho alikutwa na umauti Mei 26, mwaka huu katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar alipokuwa amelazwa baada ya
kujifungua kwa oparesheni Mei 25, mwaka huu kwenye Hospitali ya Lugalo,
Dar.
Msafara wa waombolezaji ukielekea makaburini
Jeneza lililobeba mwili wa Msanii wa bongo movie marehemu Rachel kushoto na kulia ni jeneza lenye mwili wa mtoto wa marehemu Rachel.
Baadhi ya wasanii wa Bongo movie wakiwa wamebeba majeneza yenye miili ya marehemu Rachel na Mwanae.
Baadhi ya waombolezaji.
Jeneza lenye mwili wa Marehemu Rachel
Hizi ndio nyumba za milele za Marehemu Rachel pamoja na mtoto wake.
Mchumba wa Marehemu Rachel, George Saguda akiweka udongo kwenye kaburi la Rachel na mwanae.
Mwenyekiti wa Bongo movie Steve Nyerere akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rachel na mwanae.
Irene Uwoya akiwa amezirai.
sokonejr.blogspot.com inatoa pole kwa Familia, Uongozi, wasanii na wapenzi wote wa msanii Rachel Haule.
Picha kwa hisani ya Global Publishers.