MUONGOZAJI WA FILAMU, GEORGE TYSON PICHANI AMEFARIKI!
Muongozaji wa
Bongo Movies na vipindi mbalimbali vya television hapa nchini,George
Tyson, (Baba Sonia), amefariki dunia,kwa ajali mbaya wakati akitokea
Dodoma, maeneo ya Gairo, akiwa pamoja na timu ya The Mboni Show, ambao
pia wamejeruhiwa vibaya sana.
Kwa sasa mwili wa Marehemu na majeruhi, wamepelekwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Pia kumbuka George Tysona aliwahi kuwa mme wa msanii Monalisa, na wakabahatika kuzaa mtoto mmoja anayeitwa Sonia.
Katika kuonesha ushirikiano na kuguswa na tukio msiba huo, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ambwene Yessaya AY akihesabu hela kwa ajili ya kununulia jeneza la kusafirishia mwaili wa marehemu George Tyson. AY alitoa kiasi cha shilingi laki sita Taslimu kwa ajili ya kununulia jeneza hilo.
Wakisaidiana kulibeba jeneza baada ya kutoka kulinunua.
AY, akiongozana na Rais wa shirikisho la filamu Tanzania Simon Mwakifamba wakielekea katika hospitali kuu ya Mkoa Morogoro kwa ajili ya kuuchukua mwili wa Marehemu George Tyson tayari kwa safari ya kuelekea Jijini Dare Es Salaam.