Watu wenye silaha wameshambulia Chuo
Kikuu kilichopo mji Charsadda kaskazini magharibi mwa Pakistani na
kuuwa watu 19 na wengine 50 kujeruhiwa.
Watu wanne wanaoshukiwa kuwa ni
washambuliaji wameuwawa katika mapambano ya silaha yaliyodumu kwa
muda wa saa tatu kwenye Chuo hicho Kikuu cha Bacha Khan katika mji
Charsadda.
Kumekuwepo na taarifa
zinazochanganya iwapo wapiganaji wa Kitaliban nchini Pakistan
wamehusika katika kufanya shambulizi hilo.