HALI SI SHWARI ZANZIBAR, NI BAADA YA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KUJITANGAZA KUWA YEYE NDIYE RAIS WA ZANZIBAR.
Hali ya Usalama Zanzibar sio nzuri visiwani Zanzibar, Polisi wameizingira Ofisi kuu
ya Chama Cha wananchi CUF baada ya mgombea urais wa chama hicho Maalim Seif
Sharif Hamad kujitangaza mshindi dhidi ya mpinzani wake ambaye
Dr Ally Mohamed Shein.
Gari la kikosi cha Jeshi la Polisi likiwa katika Doria.
Polisi wakizungumza na wananchi kisiwani Zanzibar
Nako katika kisiwa cha Pemba hali sio shwari katika mji wa Chake Chake, hii ni baada ya vijana wa
CUF kuingilia barabarani wakidai wanashangilia ushindi wa mgombea
wao wa Urais.
FFU wameingilia kati, wakatoa onyo wakiwataka wananchi
watawanyike lakini wakakaidi, ndipo nguvu ya ziada ya mabomu ya
machozi ilipotumika