Mwishoni mwa wiki iliyopita kaka yenu nilifunga safari kutoka hapa
'zenji' na kwenda kutembelea kule
MUHEZA moja kati ya wilaya inayopatikana katika mkoa wa Tanga.
Nilipofika jijini Dar Moja kwa moja hadi katika kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo na kuingia ndani ya basi liendalo huko nielekeako(muheza).

Mdada huyu anaitwa Monica, yeye ameniambia ni mdau mkubwa wa blogu hii. Hapa na yeye anaelekea Muheza. Je! unapenda kujua kilichofuatia baada ya hapo? ..........nifuate!!!

Hapa tupo ubungo mataa, hebu angalia foleni hiyo. Zamu yetu ilipofika tukaondoka.


Baada ya mwendo wa masaa kama mawili hivi; hatimaye tukauvuka mto
WAMI salama.

Baada ya kupita mito, misitu na nyika hatimaye nikafika Muheza. Ama kwa hakika Wilaya hii imejaliwa kwa ardhi nzuri ifaayo kwa kilimo. hakikisha hilo kupitia picha hizo hapo chini.

Hivi kweli kwa wewe mwenye akili timamu unaweza ukasema kwamba Tanzania ni nchi masikini ambayo inahitaji msaada wa chakula?

Eneo hili linaitwa Magoroto. Hebu tazama milima hiyo inavyopendeza. Wakati nashuka kutoka huko milimani nilikutana na marafiki zangu ambao nao walipenda kuuza sura na mimi katika blogu hii.

Nimepiga
'pozi' na rafiki yangu
'mgosi' Shabani a.k.a shebe.

Na huyu pia ni rafiki yangu ambaye nilimpata huko huko Magoroto
'mgosi' Muddy a.k.a Muddy guy.
Wanasema ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni. Muda wa mchana nikiwa huko huko katika milima ya usambara nilikuta watoto wakitengeneza mafuta ya mawese.
Nilipowauliza kwanini badala ya kwenda shule wao wanatengeneza mafuta walinijibu shule haina faida kwa sababu hawapati pesa.

Hicho kindoo kidogo cha lita kumi za mafuta ya mawese wanakiuza kwa shilingi elfu kumi.
HAYO NI BAADHI TU YA MAISHA YA HUKU. LAKINI JE NYUMBA ZA HUKU ZIKOJE? JAMANI WADAU HIZI NDIO NYUMBA ZA HUKU KWETU VIJIJINI AMBAKO MIMI WEWE NA HATA YULE WOTE TUMETOKEA HUKU.
NA USAFIRI WA HUKU NI HUU HAPA CHINI.