
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya hapa Zanzibar Shaka Zulu a.K.a baba Masoud akifanya mahojiano live na Hafidh Sutti 'brother Hafidh' katika studio za Zenj fm 96.8 katika kipindi cha Bongo Brain.
Kituo cha Zenj fm kimechaguliwa kuwa kituo bora cha Radio hapa Zanzibar kwa mwaka 2011.

Hapo nikila 'pozi' na mkali mwingine anayehudumu katika kituo cha radio cha Zenji fm Dj. Master Feda mwenye 'flana nyekundu'. Kushoto ni Dj. Master Feda na kulia ni mimi Dj. Master E.

Baada ya muda wa kazi kumalizika huwa jino kaka yenu huwa napenda kwenda kujipumzisha maeneo haya ya ufukweni.

Na hii ndio mandhari ya Zanzibar, mchana wa leo nilipita maeneo ya Forodhani nikaipenda sana 'taswira' hii. Jamani Karibuni Zanzibar.

Na hili ni jumba la maajabu hapa Zanzibar. 'bet el Jaib'.