Ama kwa hakika huu ni msiba wa kila Mtanzania, nadiriki kusema hivyo kwa sababu waliopoteza maisha katika meli hiyo ya Mv. Spice Islanders sio wazanzibar peke yao. meli hiyo ilipinduka ilizama usiku wa jumamosi ya tarehe 10 mwezi huu wa tisa, maeneo ya Nungwi ilipokuwa ikisafiri kutoka hapa Zanzibar na kuelekea kisiwani Pemba.
Hebu tazama baadhi ya watu katika picha hii walivyokuwa wajirajibu kuokoa maisha yao.