Mwanamuziki Mkongwe nchini aliyekuwa anatamba na staili ya kimasai ambye pia alikuwa ni mmiliki wa studio ya Motika Records iliyopo kisosora jijini Tanga Abbel Motika almaarufu Mr.Ebbo amaferiki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mfupi. Mipango ya kuusafirisha mwilli wake inafanywa ili kupelekwa Nyumbani kwao Mkoani Arusha kwa ajili ya Mazishi.
Pichani Mr. Ebbo enzi za uhai wake. Nyimbo alizotamba nazo ni pamoja na Kamongo, E omoti, bodaboda, Interview na nyingine nyingi zilizompatia umaarufu. MWENYEZI MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA ABEL MOTIKA 'Mr. Ebbo' AMINA..!!!