Etienne Tshisekedi mpinzani mkuuu wa serikali ya
katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametiwa mbaroni baada ya kuwasili
Kinshasa mji mkuu wa nchi hiyo.
Baada ya kuwepo nchini Afrika Kusini kwa muda wa
wiki mbili, Etienne tshisekedi jana alirejea Kongo.
Chama cha Umoja kwa ajili ya Demokrasia na Ustawi wa
Kijamii kinachoongozwa na mpinzani huyo mkuu wa serikali ya Kinshasa kilitoa
taarifa kikiwataka wafuasi wake kumlaki kiongozi wake huko Kinshasa.
Pamoja na
hayo yote, polisi wa mji wa Kinshasa ambao walikuwa na taarifa kuhusu
mipango hiyo ya chama cha upinzani, waliwazuia wafuasi wa mzee Tshisekedi
kuelekea katika uwanja wa ndege wa Kinshasa kwa ajili ya kumlaki kiongozi wao.
Etienne
Tshisekedi alikuwa nchini Afrika Kusini tangu Februari 25 mwaka huu kwa lengo
la kutafuta uungaji mkono wa kieneo.
Thisekedi alikuwa mpinzani mkuu wa Rais Joseph
Kabila katika uchaguzi wa rais uliopita nchini humo.