Wapiganaji wa Al Shabaab
Serikali ya Kenya imethibitisha kuwa maafisa wake wawili wa jeshi
wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa, baada ya wapiganaji wa Kiislamu
wa Al Shaabab kufanya shambulio la kuvizia, baada magari yao kukwama
barabarani huko Somalia.
Ripoti zinasema msafara wa wanajeshi wa Kenya ulikuwa ukielekea eneo la Ras Kamboni wakati shambulio hilo lilipotokea.
Kamanda wa polisi mjini Mombasa Robert Kitur amethibitisha kuwa shambulio hilo limetokea.
Kwa upande wao, msemaji wa Al shabaab, Abu Mus'ab amedai kuwa wapiganaji
wake walifanikiwa kuteketeza magari kadhaa ya jeshi la Kenya, madai
ambayo yamekanushwa vikali na utawala nchini kenya.
Aidha amesema wa wapiganaji kadhaa wa Al shabaab waliuawa na wengine kujeruhiwa wakati wa makabiliano hayo.