Mh. Mohamed Raza
Muwakilishi wa Jimbo la Uzini Zanzibar Mh. Mohamed Raza, amesema amesikitishwa sana na kitendo alichokiita kwamba si cha kiungwana kilichofanywa na mkuu wa wilaya ya kati muheshimiwa Vuai kwa kulifuta jina la mh. Raza katika orodha ya wazungumzaji kwa kumhofia mh. Raza kwa kusema ukweli juu ya matatizo ya wananchi wa eneo hilo ambao wana kero na wanahitaji misaada.
Mh. Raza amesema matatizo yote hayo yanatokana na wivu usiokuwa na maendeleo, amesema yeye ni mwananchi mwenye uchungu na nchi hii huku akisisitiza kwamba ndani ya nchi hii ya Zanzibar hakuna ubwana wala utwana kwani dhana hiyo ilishavunjwa tangu mwaka 1964 na ameahidi kuwasaidia wananchi wote bila kujali dini, kabila wala rangi zao.
Mh. Raza ameyasema hayo leo kwenye kipindi cha WASAA WA HABARI kinachorushwa na kituo cha Redio cha Chuchu fm Zanzibar.
Aidha amewapongeza mke wa Rais wa Zanzibar mama Shein pamoja na Mke wa makamu wa pili wa Rais mama Asha Balozi pamoja na baadhi ya wake wa wawakilishi.
Muwakilishi wa jimbo la uzini Mh. Mohamed Raza.