STARZ YAFIKA SALAMA SAUZI
Timu ya Tanzania (Taifa Stars) leo imetua chini Afrika ya kusini ikiwa na
wachezaji 24 kati ya 28 waliotajwa hapo mwanzoni ambao wamekwenda kuweka
kambi ya siku kumi kabla ya kuja kumenyana na Algeria Novemba 14 jijini
Dar es salaam.
wachezaji wanne waliobakia wataenda kuungana
na timu hiyo wakimaliza majukumu katika vilabu vyao wanavyochezea.
Timu ya Taifa Stars inanolewa na kocha mzalendo Charles Boniphace Mkwassa (Master)