TWIGA YAENDELEA KUJIFUA KUWAVAA MALAWI
Timu ya Taifa ya Wanawake
‘Twiga Stars’ inayonolewa na kocha mkuu Rogasian Kaijage imendelea na
mazoezi kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya
Wanawake ya Malawi utakaochezwa Novemba 07, mwaka huu jijini Dar es
salaam katika uwanja wa Azam Chamazi.
Twiga
Stars iliingia kambini Oktoba 29, katika hosteli za Shirikisho zilizopo
Karume, ina kikosi cha wachezaji 22 wanaofanya mazoezi asubuhi na jioni
katika uwanja wa Karume.
Mchezo
dhidi ya Malawi ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa, ambao kocha Kaijage
atautumia kuangalia maendeleo ya wachezaji wake kwa ajili ya maandalizi
ya michezo ya kimataifa.
Wachezaji
waliopo kambini ni Asha Rashid, Estha Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma
Omari, Mwajuma Abdallah, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Amina Ally,
Fatuma Issa, Belina Julius, Happines Hezron na Donizia Daniel.
Wengine
ni Maimuma Hamisi, Stumai Abdallah, Anna Hebron, Anastazia Anthony,
Shelder Boniface, Wema Richard, Tumaini Michael, Jane Cloudy, Saada
Ramadhani na Sofia Mwasikili.