Wahisapnia ndio wanaongoza kwa kuwa taifa la nje ya Uingereza ambalo lina wachezaji wengi ambao wamecheza EPL, hadi sasa kuna wachezaji 31 wa Hispania ambao wameshacheza katika ligi kuu ya EPL.
Katika mataifa 56 ambayo wachezaji wake wameshakwenda EPL taifa linalofuatia ni Ufaransa ambapo jumla ya wachezaji 25 kutoka nchi hiyo tayari wameshakanyaga EPL hadi hivi sasa.
Uholanzi nao wako nafasi ya tatu katika mataifa ya kigeni waliocheza EPL kwani hadi sasa Waholanzi nao wameshuhudia jumla ya wachezaji wao 22 wakisafiri hadi Uingereza kwenda kukipiga EPL.
Ubelgiji wako nafasi ya nne wakiwa na wachezaji 20 ikiwemo wawili Kelvin De Bruyne na Eden Hazard ambao kwa sasa wanatajwa kama kati ya wachezaji bora katika ligi kuu nchini Uingereza.
Jamhuri ya Ireland wako nafasi ya tano wakiwa na wachezaji 17 huku Ujerumani na Argentina wakiwa nafasi ya sita na saba wachezaji 14, Brazil nao wako nafasi ya nane na wachezaji 11.
Senegal ndio taifa linaloongoza kwa kutoa wachezaji wengi EPL ambapo hadi sasa wameshatoa wachezaji 9 na wako nafasi ya tisa huku Austria wakiwa nafasi ya kumi na wachezaji 8.
Baada ya Senegal mataifa ya Afrika yanayoongoza kutoa wachezaji EPL ni Congo na Ivory Coast ambao wametoa wachezaji 6, wakifuatiwa na Ghana 5 kisha Cameroon, Misri na Nigeria wachezaji wanne wanne.