LEO ipo Mechi moja pekee ya Ligi Kuu England ambayo itaamua nani anamaliza 2015 akiwa anaongoza Ligi.
Jana, Arsenal iliichapa Bournemouth 2-0 na kutwaa uongozi wa Ligi
wakiwa na Pointi 39 kwa Mechi 19 wakifuata Leicester wenye Pointi 38 kwa
Mechi 18, Tottenham ni wa 3 na wana Pointi 35 kwa Mechi 19 na wa 4 ni
Man City wenye Pointi 35 kwa Mechi 18.
Leo huko King Power Stadium, Leicester wanacheza na Man City na
wakishinda watarudi kileleni na wakitoka Sare watabaki Nafasi ya Pili.
Ikiwa City itashinda basi watapanda hadi Nafasi ya Pili.
Leicester wanatinga kwenye Mechi hii wakitoka kufungwa 1-0 na
Liverpool na kupoteza wimbi lao la kutofungwa katika Mechi 10 wakati
City ikiichapa Sunderland 4-1.
Wakati Leicester wana Kikosi kamili bila Majeruhi ingawa mapema
walipatwa na wasiwasi wa Staa wao Jamie Vardy, ambae ndie Mfungaji Bora
wa Ligi, kutocheza kutokana na kuugua, City watamkosa Nahodha wao
Vincent Kompany ambae ni Majeruhi pamoja na majeruhi wengine Pablo
Zabaleta, Fernando na Samir Nasri.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Leicester City: Schmeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Kante, Drinkwater, Mahrez, Albrighton, Ulloa, Vardy
Man City: Hart; Sagna, Mangala, Otamendi, Kolarov; Fernandinho, Toure; De Bruyne, Silva, Sterling; Aguero