
Elias Maguli Mchezaji wa timu ya Stand United, amekabidhiwa hundi
yake yenye thamani ya shilingi Milioni 1/= na wadhamni wakuu wa Ligi
kuu ya Vodacom Tanzania bara(Vodacom Tanzania) kwa kuibuka mchezaji bora
wa mwezi Oktoba wa Ligi hiyo.
Mchezaji huyo alikabidhiwa hundi hiyo wakati wa mazoezi yaliyokuwa
yanafanywa na timu yake katika viwanja vya JKM Park ya kujiandaa na
mchezo dhidi ya Yanga hapo kesho.