Rais wa Zamani wa Burkina faso,aliyeuliwa Thomas Sankara
Korti ya
kijeshi nchini Burkina faso imeamuru akamatwe rais wa zamani Blaise
Compaoré,kuhusiana na madai ya kuuliwa mtangulizi wakeThomas
Sankara,miaka 30 iliyopita.
Mauwaji
ya kiongozi huyo aliyekuwa na haiba,mwaka 1987 ni mojawapo ya mauwaji ya
kiajabu ajabu yaliyolikumba bara la Afrika baada ya uhuru na serikali
ya mpito ya Burkina faso imepania kujua nani walihusika.
Mabaki ya
mwili unaosemekana ni wa Thomas Sankara yalifukuliwa mapema mwaka huu
na uchunguzi kuonyesha mwili huo umejaa risasi na kwa namna hiyo
kuzidisha dhana kwamba aliuliwa kufuatia mapinduzi ya mwaka 1987
yaliyomleta madarakani Blaise Compaore.
Compaore
binafsi alitimuliwa madarakani october mwaka jana na umati wa wananchi
waliokuwa wakipinga kubadilishwa katiba ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi
ili kumruhusu aendelee kuitawala nchi hiyo baada ya miaka 27 madarakani
.Alikimbilia nchi jirani ya Côte d'Ivoire anakofikiriwa kupiga maskani
yake.
Serikali ya Côte d'Ivoire haikuarifiwa
"Nnathibitisha
jaji anaesimamia uchunguzi ametoa waranti wa kimataifa dhidi ya rais wa
zamani Blaise Compaore" amesema Prosper Farama,wakili wa familia ya
Sankara.Anasema Compaore anatuhumiwa miongoni mwa mengineyo kuhusika na
mauwaji na kusaidia kundaa mauwaji.
Duru
nyengine mbili za mahakama ambazo hazikutaka zitajwe,zimethibitisha
waranti huo wanaosema umetolewa decemba nne iliyopita.Msemaji wa
serikali hakuweza kupatikana kuthibitisha habari hizo.
Msemaji wa serikali ya Côte d'Ivoire amesema serikali yake haikuarifiwa.
Madai
dhidi ya Compaore ni hatua muhimu mbele katika kesi hiyo katika wakati
ambapo viongozi wa kipindi cha mpito wanajiandaa kumkabidhi hatamu za
uongozi waziri mkuu wa zamani Roch Marc Kabore,mshindi wa uchaguzi wa
rais wa Novemba iliyopita.
Uchunguzi wa vinasibu haukuleta matokeo yaliyotarajiwa
Thomas
Sankara aliingia madarakani kufuatia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1983 na
kufuata nadharia ya Marx pamoja na ujamaa wa kiafrika-nadharia
iliyompatia jina la "Che Guevara wa Afrika."Wasomi wengi wa Afrika
wanamwangalia Thomas Sankara kuwa ni mwanasiasa aliyekuwa akiona mbali.
Wakili
mwengine wa familia ya Sankara amesema tume ya wachunguzi wa kifaransa
wameshindwa kutathmini vinasibu vya mabaki ya mwili unaosemekana kuwa ni
wa kiongozi huyo aliyeuliwa.Familia ya Sankara wamepewa muda wa wiki
mbili zaidi kupata maoni ya tume nyengine ya wataalam.
Watuhumiwa
kumi wengine wanakabiliwa na kesi ya kuhusika na kuuliwa
Sankara.Watuhumiwa hao ni pamoja na jenerali Gilbert Diendere
aliyeongoza njama ya mapinduzi iliyoshindwa septemba mwaka huu.