MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA MADEE
Kama ulikuwa hujui basi leo nakufanya ujue kwamba mbali na masuala ya
music, msanii Madee ni shabiki wa kutupwa wa Arsenal The Gunners wale
watoto wa jiji la London pale England.
Leo Arsenal watakuwa kwenye uwanja wao kucheza ‘London Derby’ na mahasimu wao wakubwa wa jiji hilo Chelsea.
Kitu kitamu sasa kuelekea kwenye game hiyo ni pale Madee au wengi
hupenda kumwita ‘Rais wa Manzese’ alipoahidi kwamba, endapo Chelsea
itaifunga Arsenal kwenye mchezo wa leo basi yeye ataichoma moto gari
yake moja.
Leo Madee amepost ujumbe huo kwenye account yake ya instagram
unaosomeka: “Tukifungwa leo na Chelsea nachoma moto gari yangu moja”.
Madee anapata jeuri hiyo kutokana na form nzuri ya Arsenal waliyonayo
msimu huu. The Gunners wameshinda mechi saba na hawajapoteza mchezo
hata mmoja kwenye michezo tisa iliopita ya Premier League katika dimba
la Emirates huku wakiwa wameruhusu magoli manne katika mechi hizo.
Urejeo wa Mesut Ozil na Alexis Sanchez unazidi kumpa imani kubwa
Madee lakini ikumbukwe pia Eden Hazard ni sehemu ya kikosi cha Chelsea
kwenye game ya leo licha ya nyota huyo kukosa makali msimu huu.
Data zinaonesha kwamba Chelsea hawajafungwa na Arsenal kwenye mechi
nane zilizopita za Premier League. Chelsea imeshinda mechi tano na
kutoka sare mechi tatu. Arsenal imeifunga Chelsea kwa mara ya mwisho
mwaka 2011 ilipofanikiwa kupata ushindi wa goli 5-3.
Mara ya mwisho Hiddink kukiongoza kikosi cha Chelsea dhidi ya Arsenal
ilikuwa ni mwaka 2009 na akawaachia maumivu Arsenal ya kipigo kikali
kwenye uwanja wa Emirates cha mabao 4-1.
Tusubiri kuona kama Arsenal wataokoa gari la Madee isichomwe moto au Chelsea watalifanya gari hilo litiwe kibiriti.