Askofu Gilbert Deya ambaye awali
alikumbwa na kashfa ya watoto wa miujiza, amehusishwa safari hii na
miujiza feki mwingine wa kuwauzia watu mafuta ya mzaituni na kudai
kuwa yanatibu Ukimwi.
Askofu huyo ambaye alitimka Kenya na
kwenda kuishi Jijini London Uingereza baada tuhuma za kuwateka watoto
amenaswa na gazeti moja la Uingereza akiuza chupa za mafuta ya
mzaituni za mililita 750 kwa gharama ya shilingi 200 hadi 750 za
Kenya.
Mhubiri huyo mtata pamoja na
wasaidizi wake wamesema wamekuwa kiuuza mafuta hayo wanayodai kuwa
yanatibu Ukimwi, ambayo huyanunua eneo la Aldi, kwenye duka la bidhaa
kusini mwa London.