George Clooney ametoa ya moyoni juu
ya uteuzi wa waigizaji filamu wote weupe katika tuzo za Oscars, hali
iliyojitokeza kwa mwaka wa pili mfululizo na kuwabania waigiazaji
wenye asili ya Afrika.
Clooney mmoja wa waigizaji filamu
nguli, amesema ghafla tumeanza kuelekea katika mueleko usio sahihi,
na kuongeza kuwa kunawatu waliopaswa kuteuliwa kuwania tuzo hizo
ambao hawapo.
Clooney mshindi huyo wa tuzo ya
Oscar mara mbili amesema mwaka huu waandaaji wa tuzo za hizo
wamezipamgongo filamu ya nyota Will Smith ya Concussion, ya Idris
Elba ya Beasts of No Nation, Creed pamoja na Straight Outta Compton
kama filamu bora.
Kilio hicho pia cha kutopewa watu
weusi kuwania tuzo zote muhimu za filamu za Oscars pia kimemgusa
mshindi wa tuzo ya Oscar Lupita Nyo'ngo ambaye ametaka waandaaji
wafanye mabadiliko.