Kamati
ya Usimamizi wa Ligi Kuu umeagiza klabu za Polisi Tabora na Panone FC
kila moja imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa mujibu wa
Kanuni ya 14(48) kugombania kuingia uwanjani kupitia mlango wa VIP
badala ya ule wa kawaida kwenye mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya
StarTimes iliyochezwa Januari 2, 2016 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi
mjini Tabora.
Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(4) na 14(37) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Wachezaji
Ally Mwanyiro wa Rhino Rangers na Hamisi Shaban wa Lipuli wamepigwa
faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kila mmoja na kufungiwa mechi tatu kwa
kosa la kupiga wachezaji wa timu pinzani wakati wa mechi zao za Ligi
Daraja la Kwanza ya StarTimes kinyume na Kanuni ya 37(3) ya Ligi hiyo.
Pia
Polisi Mara imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya mshabiki
wao kuingia uwanjani na kumvamia mwamuzi kwa madai maamuzi yake hayakuwa
sahihi wakati wa mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes dhidi
ya Mbao FC iliyofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini
Musoma.