Zaidi
ya wanafunzi elfu 05 miamoja wa shule za msingi Wilayani Mufindi Mkoani
Iringa, wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza baada ya kufaulu
mtihani wa darasa la 07 ulifanyika mapema mwaka jana huku ufaulu huo
ukipanda na kufikia asilimia 80.39 ukilinganisha na asilimia 68.21 ya
mwaka 2014
Taarifa
ya kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri ya wilaya ya
mufindi kwa nyombo vya habari, imetanabaisha kuwa, wanafunzi waliokuwa
wamesajiliwa kufanya mtihani walikuwa elfu 07 mia mbili 20 na miongoni
mwao waliofaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari ni elfu
05 mia moja 98.
Taarifa
hiyo imeainisha mgawanyo wa wanafunzi hao kwa kuzingatia jinsi, ambapo
kati ya waliofaulu, wasichana wameongoza kwa takwimu za ufaulu huo
wakiwa elfu 02 mia nane 31 wakifuatiwa na wavulana elfu 02 mia tatu 67.
Aidha, wanafunzi wote waliofaulu wamepangiwa shule ili kuendelea na
elimu ya sekondari itakayokuwa ikitolewa bure hapa nchini.
Wilaya ya
Mufindi yenye jumla ya shule za msingi 178 imeshika nafasi ya pili
Mkoani Iringa kwa kufaulisha wanafunzi wengi kwa asilimia 80.39
ikitanguliwa na Manispaa ya Iringa iliyofaulisha kwa asilimia 80.55
ikiwa na jumla ya shule za msingi 50.