
Maafisa wa usalama nchini Kenya
wanawasaka washukiwa wanne wa ugaidi ambao wanadaiwa kukwepa msako wa
polisi katika nyumba moja Mombasa.
Polisi walipata bunduki mbili na vilipuzi baada ya kuvamia nyumba iliyokuwa ikitumiwa na wanne hao Jumatatu.
Kamishna
wa jimbo la Mombasa Nelson Marwa anasema bunduki moja iliyopatikana
ilitumiwa kumuua afisa wa polisi mjini humo mwaka uliopita.

Bunduki hiyo nyingine aina ya M4 ilitumiwa wakati wa shambulio katika kambi ya jeshi mjini Mombasa mwishoni mwa Novemba.
Polisi
wametoa picha za washukiwa hao wanne ambao wanasema ni miongoni mwa
kundi la wapiganaji wa al-Shabab waliojificha msitu wa Boni, kilomita
500 kaskazini mwa Mombasa.
Wakati wa msako huo, polisi walipata kitita cha pesa.