Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi
Kigwangalla ameagiza watanzania wote wasikubali kutozwa rushwa kwa
ajili ya damu salama na baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo
watamchukulia hatua kali.
Kauli
hiyo imetolewa mapema Januari 4 (jana) na Naibu huyo wa Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kingwangalla
alipofanya ziara katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo
jijini Dares Salaam.
Dk.
Kigwangalla amefafanua kuwa, kwa watu wote ikiwemo Nesi, Daktari ama
mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu, atachukuliwa hatua kali ikiwemo
kufukuzwa kazi.
“Kwa
watanzania wote, msikubali kutoa rushwa kwa ajili ya damu. Na kama
itatokea Nesi ama Daktari ama nani, anakuambia ulipie ili upate damu!.
Kwa sababu kuna uhaba wa damu kwa sasa.. Ripoti kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu
wa Mkoa ama Daktari Mkuu husika ama fika Wizara ya afya moja kwa moja
na kuna namba tutaitoa kwa watanzania wote mtupatie ripoti.
Mtu
atakayekutoza damu, wewe tuambie, huyo tutamfukuza kazi moja kwa moja,
hatuwezi kuendekeza watu wa namna hii... Serikali inaingia gharama kubwa
kukusanya damu kwa watu, Kuna watu wanajitolea damu zao bure.
Leo wewe
nesi ama mganga ukauze damu, hilo jambo hatutakubali hata kidogo kwa
hiyo natoa rai kwa watanzaia hiyo damu ni bure na haiuzwi na usikubali
kuuziwa damu hata kidogo.” Ameeleza hilo Dk. Kigwangalla.
Awali
katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameipongeza Ofisi ya Mpango wa Taifa
wa Damu Salama kwa kazi wanayofanya na ubunifu waliofikia wa kuhusisha
Halmshauri katika ukusanyaji wa damu huku wao wakisimamia kudhibiti
viwango vya damu ya matumizi kwa watanzania huku akitumia wasaha huo
kutoa maelekezo ya kuboresha mfumo wa motisha kwa wanaochangia damu
salama ambapo kwa wachangiaji damu kuingizwa kwenye mfumo wa
kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi
damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze
kuwa wachangiaji endelevu.
“Motisha
sio soda na maji kwa wanaochangia damu. Motisha ni hata kupewa taarifa
kwamba damu yake imesaidia kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzake aliyekuwa
anaumwa ugonjwa fulani, hii ni motisha kubwa sana kuliko hata pesa, ama
soda ama maji yanayotolewa anapochangia damu..
Lakini
kama imeshajitokeza mtu kuwa na tabia ya kuchangia damu, huyu sio wa
kumpoteza, maana yake kuna uwezekano mkubwa wa akarudi tena kuchangia
damu, mtu huyu ni lazima kuwe na mfumo wa kielekrioniki wa komputa wa
kumtakia salamu, taarifa na anakuwa kwenye database yenu.