
Hiyo ni ndege aina ya boeing 777 ya shirika la ndege ya Continental ya nchini Brussels yenye namba za usajili 61 ambayo rubani wake amekufa huku ndege hiyo ikiwa angani ikitokea Brussels kuelekea New York.
Maofisa wa mamlaka ya hali ya hewa wa Marekani wamesema kwamba baadaya kutokea kifo hicho ndipo msaidzi wa rubani huyo ikambidi abebe jukumu la kuiongoza ndege hiyo na kufanikiwa kuifikisha salama kwenye uwanja wa ndege wa Newark uliopo nje kidogo ya jiji la New York.
Aidha shirika hilo limesema kwamba rubani huyo mwenye umri wa miaka 60 amelitumikia shirika hilo kwa muda miaka 30 akiwa kama rubani.