
Huko congo ya mashariki kambi moja ya umoja wa mataifa imeshambuliwa na kundi la wanajeshi linalolalamika kutokulipwa mishahara.
Mashambulizi hayo ni moja ya misururu ya mashambulizi ya wanajeshi walioasi huko kasikazini mwa kivu ambao hawajalipwa mishahara yao kwa kipindi cha takribani miezi sita.
Msemaji wa umoja wa mataifa amesema kuwa hali hiyo inahitaji kushughulikiwa kwa haraka, lakini pia amesema makamanda hao wanapesa ila hawataki tu kuwalipa mishahara wanajeshi hao.