
Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk.Aman Abeid Karume jana amezindua maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma jijini Dar Es Salaam, ambayo yanashirikisha taasisi 170 za serikali kutoka hapa nchini wakati taasisi 21 zinatoka katika nchi jirani ya Kenya.
Kwa mujibu wa msemaji wa rais menejimenti ya utumishi wa umma Zamaradi Kawawa amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kuwaeleza wananchi kazi mbalimbali zinazofanywa na serikali ikiwa ni pamoja na kupokea kero za wananchi katika utendaji wa serikali.
Maadhimisho hayo ambayo yanataraji kumalizika juni 23 yanashirikisha jumla ya nchi 14 zikiwemo Namibia, Afrika ya kusini pamoja na Zimbabwe.