Sanaa ni kazi kama vile kazi nyingine, na wengine kwa sanaa hiyo hiyo kwao ni kipawa ambacho wamejaaliwa na Mwenyezi Mungu.
Amini usiamini kwamba wapo watu wanaitegemea sanaa katika kuendesha maisha yao.
Hapa namaanisha watu wanasomesha watoto zao, wanavalisha familia zao na hata mwisho wa siku watoto wao wanakuwa na ujunja kama sio nguvu za kuweza kupishana chooni.
Mtu kama Kingwendu ngwendulilekabla hajafanya chochote ukimuona tu yeye mwenyewe ni kichekesho, lakini hiyo ni sanaa ambayo kwake ni ajira.
HEBU MUANGALIE NA HUYU HAPA CHINI.

Huyu mnyamwenga hilo domo lake lina lastiki au vipi?
Mimi nadhani watu kama hawa ndio wale wanaoambiwa domo kubwa chapati hukunji.
HAAA.! NA HUYU ANALIA AU ANACHEKA?
Eti, huyu ni mwanamke au mwanaume?
kazi kwako mdau.