
Hili ndilo kundi mahiri la muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania a.k.a bongofleva lenye maskani yake pande za Temeke WANAUME HALISI ambalo linataraji kuondoka nchini mwanzoni mwa mwezi julai kuelekea nchini Dubai kwa ajili ya kupiga shoo kadhaa za kiukweli zaidi.
Wanaume Halisi wamepata shavu hilo kutoka katika kampuni ya Consult LB nchini humo.