
LEO patakuwa hapatoshi katika dimba la Taifa jijini Dar Es Salaam kati timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Starz na New Zealand kipute kitakachopigwa saa moja za usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki. Kocha Mkuu wa Starz Mbrazil Maxio Maximo huenda leo akasafisha jina na kulifukuza 'BUNDI' linaloendelea kumuandama katika timu hiyo.
Mbrazili huyo ana kila sababu ya kuhakikisha leo timu yake inafanya vizuri ili kurejesha imani ya watanzania ambayo imeanza kupotea kama sio kufutika kabisa.
Hapo juu kaka mkubwa(MAXIO) akiwa mazoezini na vijana wake katika uwanja wa Karume.
Kaka mkubwa a.k.a (Maxio maximo) akilonga na na waandishi wa habari huku pembeni yake kocha mkuu wa New Zealand Ricki Herbet akimsikiliza kwa makini.

Hii ndio Nationa Stadium mpya itakayowaka moto usiku wa leo
Hao ni wapiganaji wetu kumi na moja watakao ipeperusha bendera yetu usiku wa leo.

Athuman Idd 'chuji' mwenye uzi wa bluu katika moja heka heka za kutafuta goli.
KILA LA HERI STARZ.