
Nilipata bahati ya kuzungumza nae manbo kibao kuhusiana na maisha yake kwa ujumla pamoja na kipaji chake.
Jina lake ni Charles Francis a.k.a C9, ukipenda muite C kenda.
Mwana kafaka huyu ni bonge la mtayarishaji wa muziki hapa nchini a.k.a prodyuza ambaye alianzia kazi hiyo ndani ya studio za Maconellah Recz iliyoko pande za kwa Mchina Zenji na kufanikiwa kuunyanyua na kuuweka katika levo ya juu muziki wa kizazi kipya zenji pamoja na Tanzania kwa ujumla, lakini kwa sasa yupo pande za bongo.
Ki ukweli yupo juu sana kwani yeye mwenyewe anagonga kibodi, gitaa na kila kitu.
Nilipomuuliza kwa nini ameamua kujiita C-9 aliniambia amependa kujiita hivyo kwa sababu yeye ni mtoto wa tisa kuzaliwa katika familia yao.
Ukiachia mbali kufanya kazi kama muziki prodyuza lakini pia ameshawahi kufanya kazi katika kituo maarufu cha radio Zanzibar cha 90.9 CHUCHU FM kama radio prodyuza.

Hapo C-9 akitoa inrtodaksheni katika hemkwa 2008/9 kushoto yake ni braza nanihii.
Blogu hii inamtakia kila la heri pamoja na mafanikio tele C-9