Kaka yenu mwanzoni mwa wiki hii nimekutana na kitu ambacho kimenifanya nisiamini macho yangu baada ya kuona braza mmoja amewekewa ngumu na dingi yake kumuoa msichana ambaye yeye ndiye chagou lake, eti kwa kuwa yule dingi hajampenda mkwewe mtarajiwa au labda kutokana na sababu zozote zile ambazo mimi na wewe hatuzifahamu.
Mimi kwa mtazamo wangu wazee hebu mbadilike kwasababu hamjui hao watoto wenu wametoana wapi.
Na makabila pia yasiwe kisingizio kwa hizo mila zenu tasa. Nawaombeni sana, wahehe, wasukuma, wabondei, wafipa, wachaga, na makabila yote yaliyopo Tanzania pamoja na
'WAKWE ZANGU WAPARE' mbadilike na mziache mila hizo mbovu. Au mdau wa blogu hii wewe unaitizamaje ishu hii.????