Jana usiku yapata muda wa saa mbili kule Gongo la Mboto katika kambi ya jeshi kumetokea milipuko ya mabomu iliyodumu kwa usiku kucha, huku wakaazi wengi wa maeneo hayo wakipata ulemavu, vidonda, na hata wengine kupoteza maisha yao.
Waziri wa Ulinzi Dk. Hussein Mwinyi akizungumza na Mkuu wa JWTZ Jenerali Davis Mwamunyange na mnadhimu wa jeshi hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete hapo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua eneo la tukio katika kambi ya JWTZ ukonga jijini Dar Es Salaam ambako jana usiku kumetokea milipuko ya mabomu.
Huyu sio mama yake la hasha! Ni Daktari wa hospitali Amana akiwa na mtoto huyo ambaye amepotezana na wazazi wake.
Watu wakidandia lori kwa kujisalimisha na milipuko hiyo iliyotokea jana Gongo la Mboto Dar Es Salaam.
Nyumba nyingi za wananchi wa maeneo mengi zimebomoka kufuatia kulipukiwa na mabomu hayo, kiasi cha kuwafanya kuzikimbia nyumba zao na kuweka kambi katika uwanja wa mpira (uwanja wa uhuru).
Hilo ni baadhi ya bomu ambalo limelipuka huko Gongo la Mboto Jijini Dar Es Salaam
Baadhi ya majeruhi wakiwa katika hospitali yaTemeke wakipatiwa matibabu baada ya
kujeruhiwa na milipuko ya mabomu iliyotokea kule Gongo la Mboto jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya majeruhi wakifikishwa katika hospitali ya Amana jana usiku baada ya kukutwa na milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi ya jeshi ya Gongo la mboto jijini Dar Es Salaam jana usiku.
Pichani ni baadhi ya watoto waliookotwa Gongo la Mboto kutokana na kukimbiwa na wazazi wao kukimbilia sehemu isiyojulikana kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea kule katika kambi ya jeshi la wananchi(JWTZ) Gongo la Mboto jijini Dar Es Salaam.