
Mnajimu maarufu wa Afrika Mashariki Sheikh Yahya Hussein, amefariki dunia asubuhi ya leo nyumbani kwake jijini Dar Es Salaam, kwa maradhi ya moyo.
Sheikh Yahya alizaliwa mwaka 1932 kule katika wilaya ya bagamoyo mkoa wa Pwani.
Marehemu Sheikh Yahya ameacha mjane na watoto 20.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi. Amen.!