Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza ni kitu gani kinachosababisha timu yetu ya Taifa kuboronga katika michezo ya kimataifa lakini sipati nimekuwa jibu. Kama Uwanja mzuri tunao, wadhamini wapo tena wa kutosha na wameonesha mchango wao mkubwa katika soka la bongo, Mwalimu mzuri yupo sasa tatizo kubwa ni nini?

Hao ni wachezaji wa timu ya Taifa Stars walipokuwa wakisalimiana na wachezaji wa Bafana Bafana katika dimba la Taifa kabla ya kupepetana ya Timu hiyo ya Bafana Bafana kutoka kule South Africa 'bondeni' ambapo Stars ilichapwa bao 1-0.

Kiungo wa Stars Mohamed Banka akijaribu kumtoka mchezaji wa Bafana Bafana.