
Asalaam Aleykum, Amani iwe juu yako mdau.
Kifupi napenda kuwaambia kwamba baada ya kushinda na kuwa Radio ya kwanza kwa ubora hapa kisiwani Zanzibar, hatimaye Zanzibar Media Corporation Ltd, inayomiliki kituo cha radio cha Zenj fm 96.8 na gazeti la Nipe Habari. imewaandalia semina wafanyakazi wake wote namaanisha watangazaji na waandishi wa habari wa Radio hiyo kwa ajili ya kujifua na kujipiga msasa. Semina iliyoanza leo tarehe 8-9 mwezi huu, inayofanyika katika Hoteli ya kitalii Visitors Inn Hotel - Jambiani Zanzibar Kwa kufunguliwa na Waziri wa habari utamaduni na utalii Zanzibar Abdillah Jihadi Hassan. Semina hiyo inaongozwa na wakufunzi waliobobea katika fani ya habari kama vile Abdallah Majura, bi. Edda Sanga na Ahmed Kipozi wengine ni Salim Said Salim, na Mtaalamu wa kiswahili kutoka hapa Zanzibar Amour Abdallah Khamis.
Kwa habari zaidi na picha za matukio endelea kutembelea blogu hii.!!!!!!!!