KIKOSI CHA BRAZIL
HATIMAE, Fainali za Kombe la Dunia zinaanza Leo hii huko Sao Paulo, Brazil wakati Wenyeji Brazil
wataivaa Croatia katika Mechi ya Kwanza ya Kundi A itakayochezwa Arena
Corinthians, au kwa Jina jingine Arena de Sao Paulo.
Kihistoria Mechi ya Ufunguzi huwa ngumu kwa Wenyeji na mara nyingi huanza vibaya kwa Sare au hata kufungwa.
Je hii ya Leo itakuwaje?
Hali za Timu
Meneja wa Brazil, Luiz Felipe Scolari,
anatarajiwa kuutumia Mfumo wa 4-2-3-1 lakini hamna uhakika kama Kiungo
wa Chelsea, Oscar, anaweza kuanza kutokana na fomu yake kuporomoka hivi
karibuni.

Lakini asipocheza Oscar, Mchezaji mwingine wa Chelsea, Willian, huenda akajaza nafasi yake.
Croatia wanatinga kwenye Mechi hii
wakiwa na pigo kubwa la kumkosa Mario Mandzukic ambae yuko Kifungoni
baada ya kupewa Kadi Nyekundu kwenye Mechi yao ya Mchujo dhidi ya
Iceland Mwezi Novemba.

Hata
hivyo, Croatia wanae Eduardo, Mzaliwa wa Brazil, ambae ameungama
akiwepo huenda akaimba Nyimbo za Taifa zote mbili ambazo huimbwa kabla
Mechi kuanza.
Mvuto mkubwa kwa Duniani nzima ni kutaka
kumwona Supastaa mdogo wa Brazil, Neymar, atachezaje na kama ataweza
kurithi mikoba ya Lejendari Pele kwa kuwika kwenye Kombe la Dunia na
kuipa Nchi yake Taji.
Uso kwa Uso
Brazil na Croatia zimeshawahi kukutana
mara mbili na Brazil kushinda mara 1, Bao 1-0 huko Germany kwenye
Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2006 kwa Bao la Kaka na kutoka Sare 1-1
Mwaka 2005 kwenye Mechi ya Kirafiki.
Takwimu za Mechi
Wakielekea Kombe la Dunia, Brazil
wamekuwa wakifunga Watani wa Bao 2.58 kwa Gemu, wakifunga Bao 2 au zaidi
katika Asilimia 84 ya Mechi zao..
VIKOSI VINATARAJIWA:
Brazil (Mfumo: 4-2-3-1): Cesar; Alves, Luiz, Silva, Marcelo; Gustavo, Paulinho; Hulk, Oscar, Neymar; Fred.
Croatia (Mfumo: 4-2-3-1): Pletikosa; Srna, Lovren, Corluka, Pranjic; Vukojevic, Modric; Perisic, Rakitic, Kovacic; Olic.
Refa: Yuichi Nishimura (Japan)