PETE WAANZISHA MRADI WA UFUGAJI VIPEPEO
Wananchi wa kijiji cha pete wameamuwa kuanzisha
mradi wa ufugaji wa vipepeo ili kuweza kujiajiri na kuondokana na umasikini.
Wakizungumza na chuchu fm ali amer simai ambae
ni miongoni mwa wafugaji wa vipepeo amesema lengo la kuazishwa mradi huo ni
kupunguza uharibifu wa misitu ambao ni rasilimali ya taifa.
Amesema ufugaji wa vipepeo unafaida kubwa
hususan kipindi cha mvua ambapo vipepeo huzaliwa kwa wingi.
Amewataka wananchi wa kijiji hicho hasa vijana
kujikita katika mradi huo ili kuweza kuondokana na ukosefu wa ajira na
kuepukana na uharibifu wa msitu kwa kukata miti.
Nae Fred Stamila ambae ni mnunuzi wa vipepeo
amesema mradi huo umekuwa ukiwanufaisha wananchi wanaojishughulisha na ufugaji
huo kwa kuendeleza familia zao katika mahitaji mbalimbali.
Mradi wa vipepeo umeanzishwa mwaka 2004 kwa
lengo la kuulinda na kuutunza msitu wa taifa wa jozani ambapo wananchi wa
maeneo hayo na maeneo jirani walikuwa wakiuhujumu kwa kukata miti kwa ajili ya
shughuli mbalimbali za kijamii.
WANANCHI WA
KASKAZINI B WAILALAMIKIA ZAWA
wananchi
wa shehiya ya
kilombero, wilaya ya
kaskazini b unguja ,wameilalamikia mamlaka
ya maji zawa,kutokana
na kukosa huduma
ya maji katika kijiji
chao.
wakizungumza na
chuchu fm wananchi
hao,wamesema ni muda
mrefu kwa sasa
wamekuwa waki ihangaikia huduma
hiyo,kitu ambacho kinawapelekea kuchukua
umbali wa maili
tatu kuelekea vijiji
vya jirani.
nae
sheha wa shehiya
hiyo ya kilombero ,amour foum
khamis amethibitisha kuwepo
kwa tatizo hilo,
na kuiyomba serekali
iwatafutie ufumbuzi wa haraka
ili huduma maji kupatikana kijijini hapo.
NAPE: LENGO LA
UKAWA NI KUFICHA MIGOGORO CHADEMA
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,
ametoboa siri kwamba, viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema wamelazimika
kukumbatia kinachoitwa Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA), ili kujaribu kupoza
migogoro iliyopo ndani ya chama hicho ambayo inakiua.
Amesema, siyo kweli kwamba Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Woilbrod Silaa na
Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe wanahangaika na muungano huo unaoitwa
wa kutafuta Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa lengo la kusaidia wananchi bali ni
kujaribu kupoza makali, baada ya kuona kwamba chama chao kimo katika mgogoro
mkubwa wa ndani ambao si mda mrefu utaua.
"Chadema wapo katika mgogoro mkubwa kutokana na baadhi ya viongozi wake
hasa wa ngazi za juu kukiendesha chama katika misingi ya ubaguzi.. na ndiyo
sababu leo au hata kesho, Mbowe hawezi kuitisha kikao cha Baraza Kuu la chama
hicho, na akijaribu kufanya hivyo anatimuliwa", alisema Nape.
Nape pia hakumuweka kiporo Mbunge wa jimbo la Ubungo, John Mwinyika, badala
yake alimpasha kwenye mkutano huo kwamba, baada ya wananchi wa jimbo hilo
kudanganyika na kumpa ubunge, sasa akae mkao wa kuondoka baada ya uchaguzi mkuu
utakaofanyika 2014.
"Mnyika na Chadema yake tunawambia pango lao hapa jimbo la Ubungo
linamalizika rasmi mwaka 2014 na hatuma mpango wa kumuongezea, kilichobaki sasa
ajiandae tu kuondoka taratibu", alisema Nape.
Alisema, Mnyika kama walivyo wabunge katika maeneo ambako wananchi walijaribu
kuwachagua wapinzani, anachofanya yeye na Chama chake cha Chadema ni kupambana
na kujenga misingi ya chama chao kuendelea kuwa kuishi na kamwe hawashughulikii
matatizo ya wananchi.
"Na hili niliwaambia miaka mingi iliyopita, nilisema hapa ubungo kwamba
mkimchagua mpinzani kazi yake itakuwa kutafuta njia za kuimarisha chama chake,
na kamwe hataweza kujihusisha na masuala ya maendeleo yenu", alidai Nape
na kuongeza;-
"Mnyika kama kweli una lengo la kuwatumikia wananchi wa Ubungo, umefika
wakati wa kuacha sasa na mambo ya kudai kila mara hoja binafsi bungeni, sasa
udai na hoja za wananchi, maana ukiendelea kudai hoja binafsi zaa wananchi
utadai lini?"
Alisema, ni kutokana na wapinzani akiwemo Mnyika na chama chake cha Chadema,
kutokwa mapovu midomoni kila kona ya nchi wakihangaika na Katiba mpya, tena
wanachozungumzia zaidi serikalikali tatu na kusingizia kwamba ndiyo mahitaji ya
wananchi huku wakijua wazi kwamba wanachohitaji wananchi kama wa Ubungo ni
maji, elimu na afya na siyo idadi ya serikali.
Nape alisema hivi sasa wananchi wameshastukia vyama vya upinzani kwamba vipo
kwa maslahi ya wachache ni si ya wananchi kama vinavyovyojinadi.
Alisema, miongoni mwa dalili za wananchi kuvistukia vyama cya upinzani, ni hali
ilivyojitokeza wakati wa ziara za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
alkizofanya akiambatana na Nape mwenyewe mikoani.
Nape alisema, katika ziara hizo hadi sasa wanachama 12, 430 walijiunga
CCM huku karibu nusu yao wakiwa wametoka katika vyama vya upinzani vikiwemo
Chadema na CUF.
Katika mkutano huo ulioandaliliwa na Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam,
Nape alipokea wanachama wapya 480, wengi wao wakiwa wamehamia CCM kutoka katika
vyama vya Chadema na CUF kwa nyakati tofauti.
CUF
KINAENDELEA NA MAANDALIZI YAKE KWA AJILI YA MKUTANO MKUU TAIFA
Chama Cha Wananchi CUF
kinaendelea na maandalizi yake kwa ajili ya Mkutano Mkuu Taifa utakaoambatana
na uchaguzi wa viongozi wakuu wa Kitaifa wa Chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi kuu za Chama hicho Buguruni Dar
es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad amesema
maandalizi yote ya msingi kwa ajili ya mkutano huo yamekamilika.
Maalim Seif
amesema katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 hadi 27 mwezi huu,
wajumbe wa mkutano watapokea taarifa mbali mbali za kazi za chama kuanzia mwaka
2009 hadi 2014 ambapo pia watapata fursa ya kuzijadili.
Amebainisha
kazi nyengine za mkutano huo kuwa ni pamoja na kuwachagua viongozi wakuu wa
kitaifa wa chama hicho ambao ni Mwenyekiti wa Taifa, Makamu Mwenyekiti na
Katibu Mkuu.
Viongozi wengine watakaochaguliwa katika mkutano huo ni wajumbe wa Baraza Kuu
la uongozi taifa pamoja na wajumbe wa viti maalum vya wanawake.
Maalim Seif
amesema kwa sasa Chama hicho kinaendelea na vikao mbali mbali kikiwemo cha
kamati tendaji, ikiwa ni maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mkutano huo ambapo
wajumbe wote wa mkutano kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watakuwa wamewasili
ifikapo tarehe 22/06/2014 kwa ajili ya mkutano huo wa kitaifa.
Wakati huo
huo Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Prof. Ibrahim Lipumba ameichambua bajeti ya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2014/2015, na
kusema kuwa ina mapungufu mengi.
Prof. Lipumba amewaambia waandishi wa Habari kuwa bajeti ikiwa nyenzo muhimu ya
sera za serikali, inapaswa kuandaliwa kwa umakini ili iweze kutekelezwa kwa
mujibu wa mahitaji yaliyopo.
Amesema ni
jambo la kushangaza kuona bajeti inayoidhinishwa katika bunge kila mwaka
haitekelezwi kama ilivyopangwa, na badala yake kunakuwa na tofauti kubwa kati
ya bajeti inayoaishinishwa na ile inayopatikana kwa matumizi ya mwaka.
Amesema
baadhi ya Wizara za Serikali zimekuwa zikipata fedha chini ya asilimia 50 ya
matumizi yaliyopangwa, na kusababisha miradi mingi ya maendeleo kuzorota
kutokana na ukosefu wa fedha.
Aidha amesema bajeti hiyo bado inabakia kuwa tegemezi kutokana na mapato ya
ndani kuwa madogo ikilinganishwa na matumizi ya kawaida ya serikali.
Prof.
Lipumba amefahamisha kuwa serikali inapaswa kujipanga ipasavyo, ili kuepuka
utegemezi kwa bajeti ya maendeleo ambapo amesema imekuwa ikitegemea zaidi
misaada na mikopo kutoka nchi za nje na mashirika ya Kimataifa.
Ametaja
mambo ya msingi yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa utayarishaji wa bajeti kuwa
ni pamoja na bajeti kuweza kufikia malengo ya uchumi mpana, ukuaji wa pato la
taifa, mfumko wa bei, akiba ya fedha za kigeni pamoja na thamani sarafu.
Mambo
mengine aliyobainisha ni ni kutaka matumizi yagawiwe kulingana na malengo ya
sera ya taifa pamoja na kujenga mazingira ya utekelezaji mzuri wa bajeti.
Katika hatua
nyingine Prof. Lipumba amesema bado bajeti hiyo haijaweka bayana juu ya ukuwaji
wa deni la Taifa ambalo amesema limekuwa likikuwa kwa asilimia 20 kwa mwaka
wakati ukuaji wa uchumi ni asilimia 7 kwa mwaka.
Amesema deni
hilo ni hatari kwa Taifa na linapaswa kuwekewa mikakati imara ili lisiendelee
kuongezeka na kudumaza pato la wananchi.
Amesema licha ya serikali kusema bajeti imelenga kupunguza gharama za maisha
kwa wananchi, lakini wananchi walio wengi bado wanaona kuwa gharama za maisha
zinaendelea kupanda kwa kasi kubwa kuliko takwimu zinazotolewa na serikali.
MRADI WA PROSPER KURUDISHA SHULENI WATOTO WALIOKOSA ELIMU
SIKONGE WAPONGEZWA
MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge
mkoani Tabora Robert
Kamoga amepongeza jitihada zinazofanywa na mradi wa PROSPER katika
kutokomeza utumikishwaji watoto katika shughuli za kilimo huku akisifu
utaratibu wa kurudishwa shule watoto wote waliokosa nafasi hiyo.
Kamoga ametoa pongezi hizo alipokuwa akizungumza na mamia ya
wananchi
waliojitokeza katika maadhimisho ya siku ya kupinga utumikishwaji
watoto iliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Udongo kata ya Ipole
wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
Alisema mradi huu unastahili kupongezwa kwa sababu mkoa wa Tabora
ni
miongoni mwa mikoa 5 inayoongoza kwa umaskini hapa nchini na asilimia
kubwa ya wananchi wake ni maskini hali inayochangia watoto wengi
kutumikishwa katika kazi ngumu kwa ujira mdogo.
Mradi huu ni mkombozi kwa watoto wadogo kwa sababu wazazi wengi
walikuwa hawawapeleki shule kwa kisingizio cha umaskini na badala yake
wanawapeleka shambani wakawasaidie kulima tumbaku au kuchunga ng’ombe,
alisema.
Kamoga aliongeza kuwa utumikishwaji watoto ni hatari sana katika
ustawi wao kwa sababu huwakosesha fursa mbalimbali katika makuzi yao
ikiwemo haki ya kupata elimu na malezi bora. "Wataalamu wanasema ukimnyima
mtoto haki zake anaathirika kisaikolojia
mpaka ukubwani mwake na watoto ndio taifa la leo na kesho, hivyo
wanapaswa kulindwa, kutunzwa na kupendwa, kwa kufanya hivyo tutakuwa
tunajenga taifa kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa, alifafanua.
Aidha alisema sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 kifungu cha
78 (1)
inakataza mtu yeyote kuajiri au kutumikisha watoto katika shughuli
yoyote ile inayowaadhili watoto hao, hivyo kumtumikisha ni kwenda
kinyume na sheria za nchi anapaswa kushitakiwa mara moja.
Kamoga alisema PROSPER imefanikiwa kuwarudisha shuleni watoto
wengi
sana waliokosa elimu katika wilaya za Sikonge na Urambo na
kuwagharamiwa masomo yao kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba huku
vikundi mbalimbali vya vijana na akina mama vikipewa mafunzo ya
ujasiriamali, kilimo, ufugaji na mikopo kwa lengo la kuwawezesha
kiuchumi.
Mradi huu umefanya kazi nzuri sana katika vijiji 20 vilivyoko
katika
wilaya hizo, Mkurugenzi (Bahati Nzunda) naomba uangalie uwezekano wa
kupanua huduma hii katika vijiji vingine kwani wapo watoto wengi sana
walioathiriwa na utumikishwaji huu, aliongeza.
Ili kudhibiti vitendo hivyo, Kamoga aliagiza waalimu wakuu wa
shule
zote za msingi katika wilaya hiyo kuhakikisha wanafuatilia mahudhurio
ya watoto shuleni ili kubaini watoto wasiofika shule ili wazazi wao
wakamatwe mara moja na kutozwa faini.
Sambamba na hilo aliagiza watendaji wote wa halmashauri kuanzia
ngazi
ya vijiji na kata kuwachukulia hatua kali watu wote watakaobainika
kujihusisha na vitendo vya utumikishwaji watoto katika maeneo yao huku
akiomba asasi zingine kuunga mkono jitihada hizo.
SAUDI ARABIA YAKATAZA VIBARUA
JUANI
Sheria mpya za kazi
zimeanzishwa nchini Saudi Arabia kwa watu wanaofanya kazi nje, kwenye jua.
Kutoka sasa hadi September, vibarua
hawaruhusiwi kufanya kazi nje kutoka saa 6 mchana hadi 9 jioni, kwa sababu ya
masilahi ya afya yao.
Wafanyakazi kwenye mitambo ya mafuta na kazi
za lazima za ukarabati, hawahusishwi na uamuzi huo ikiwa hatua zinachukuliwa
kuwakinga na jua.
Nchi jirani ya Qatar, imelaumiwa sana kwa
kuwalazimisha vibarua kutoka India kufanya kazi kutwa nje, wakijenga mwahala
mwa mashindano ya kandanda ya mwaka wa 2022.
Imesema itachukua hatua kufanya mazingira yao
ya kazi kuwa bora.
SADIQ AL-MAHDI AFUNGULIWA SUDAN
Wakuu wa Sudan wamemuachilia
huru kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Sadiq al-Mahdi, ambaye alikamatwa
mwezi May kwa mashtaka ya kuchochea chuki dhidi ya taifa.
Adhabu ya mashtaka hayo yanaweza kuwa kifo.
Bwana al Mahdi, ambaye anaongoza chama cha
Umma, alilalamika juu ya sera za serikali kuhusu Darfur na alishutumu wanajeshi
wa serikali kuwa wanakiuka haki za kibinaadamu, pamoja na ubakaji.
Waziri wa Habari wa Sudan, Yasser Youssef,
alisema Sadiq al-Mahdi aliachiliwa huru kufuatana na sheria za nchi, lakini
hakueleza zaidi.
RAIS ROUHANI AONANA NA
MASHABANE MJINI TEHRAN
Rais Hasan Rouhani amesema kuwa, vikwazo vya
kidhulma dhidi ya Iran havikubaliki na ndio maana mashirika ya Magharibi hivi
sasa yanafanya mazungumzo na kuweka mikataba ya ushirikiano na Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran.
Rais Rouhani amesema hayo jana mjini Tehran
wakati alipoonana na Waziri wa Mashauriano ya Kigeni na Uhusiano wa Kimataifa
wa Afrika Kusini, Bi Maite Nkoana-Mashabane.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia
ameipongeza Afrika Kusini kwa msimamo wake kuhusiana na miradi ya amani ya
nyuklia ya Iran na kusisitiza kuwa, taasisi ya vikwazo viovu na vya kidhulma
vilivyowekwa na nchi za Magharibi dhidi ya Iran inaandamwa na matatizo mengi sana.
Aidha amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
iko tayari wakati wote kwa ajili ya makubaliano ya mwisho ya mazungumzo ya
nyuklia baina yake na kundi la 5+1 kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Vile vile ameipongeza Afrika Kusini kwa
mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 20 wa ukombozi wa taifa hilo kutoka katika
makucha ya makaburu baada ya wanamapambano wa nchi hiyo wakiongozwa na kiongozi
shujaa hayati Nelson Mandela kuushinda utawala wa kibagu nchini humo. Ameongeza
kuwa, mapambano ya wananchi wa Afrika Kusini yameandaa uwanja mzuri wa kiroho,
kisaikilojia na kiutamaduni wa kuweza kudumisha ushirikiano baina yake na taifa
la Iran.
SHAMBULIO LA KUVIZIA
LAUWA WATU 7 NCHINI YEMEN
Wahudumu wa tiba saba wameuawa na wengine
kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la kuvizia katika basi lao huko kaskazini
mwa Yemen. Watu saba hao walipoteza maisha baada ya basi walilokuwa wamepanda
kushambuliwa ghafla kaskazini mwa Aden wakati walipokuwa wanaelekea katika
hospitali moja ya jeshi.
Basi hilo lilikuwa limewapakia madaktari na
wauguzi wanaofanya kazi kwenye hospitali moja ya jeshi huko Aden. Mwanamke
mmoja ni miongoni mwa wahudumu hao saba wa tiba waliouawa leo katika shambulizi
la kuvizia kaskazini mwa Aden huko Yemen.
Watu 11 wengine wamejeruhiwa kwenye shambulio
hilo. Maafisa wa Yemen wanaamini kuwa, wapiganaji wa mtandao wa al Qaida
wamehusika na shambulio hilo. Itakumbukwa kuwa Waziri wa Ulinzi wa Yemen tarehe
5 mwezi uliopita wa Mei alinusurika kuuliwa katika shambulizi la kuvizia dhidi
ya msafara wake. Yemen ambayo inapakana na Saudi Arabia ni ngome ya mtandao wa
al Qaida katika rasi ya Bara Arabu.