WENYEJI
Brazil, wamelazimishwa safe ya bila kufungana na Mexico katika mchezo
wa Kundi A Kombe la Dunia uliomalizika muda mfupi uliopita.
Brazil
wakiongozwa na nyota wake, Neymar walicheza vizuri na kushambulia mno
langoni mwa wapinzani wao hao wa Amerika Kusini pia, lakini wakakosa
bahati ya kufunga.
Timu
hiyo inayofundishwa Luiz Felipe Scolari ilifanya jitihada nyingi za
kufunga kwa kutengeneza nafasi nyingi, lakini sifa zimuendee kipa wa Mexico, Guillermo Ochoa, aliyeinusuru timu yake kwa kuokoa mabao mawili au matatu ya wazi mno.
KIPA WA MEXICO GUILLERMO OCHOA
ANDRES GUARDADO AKIJARIBU KUMZUIA NEYMAR