Ni
muhimu sana kwako mwanaume kujua kwa uhakika kuwa mwanamke anakupeda
kweli kweli,utajuaje kuwa mwanamke anakupenda? Zifuatazo ni ishara
ambazo wewe kama mwanaume unapaswa uwe makini ili uweze kuziona na
haraka kumtolea uvivu huyo mwanamke.
1Mwanamke anayekupenda atahangaika juu yako, atahangaika juu ya usalama
wako,raha yako,heshima yako na maendeleo yako.Hii ni moja kati ya ishara
kubwa kuwa mwanamke huyo anaupendo na wewe.
2 Mwanamke anayekupenda atakuonea wivu mara kadhaa,Wivu ni ishara kuwa
anakupenda wewe na anataka akulinde usiibiwe au asije
akakupoteza,anaogopa usije ukatoka katika maisha yake,au kwa maneno
mengine usije ukamtoa moyoni mwako na nafasi yake ikachukuliwa.Japo wivu
ukizidi sana pia inaweza kuleta tatizo.
3 Mwanamke anayekupenda atakapokuwa mbele ya marafiki zake au watu
wengine atacheka nao lakini atakugeuzia ww macho/uso wake haraka sana.
Kufanya hivi ni kuonyesha kuwa anakuhesabia ww kuwa utaweza kumletea
furaha katika maisha yake,zaidi ya hilo ni kwamba anatumaini kuwa
utamuona kuwa yeye ni mtu aliye rahisi kufurahishwa kwa kuwa yeye ni mtu
wa furaha.
4 Mwanamke anayekupenda ataendelea kukuangalia usoni kwa muda mrefu
kuliko ilivyo kawaida ya wanawake wengine,mara nyingi atakuangalia na
kutabasamu vizuri. Hii huenda ni ishara moja muhimu sana ya kukuambia
kuwa “NJOO NIKO KWAAJILI YAKO.”
Hivyo kama ulikuwa
unahisi unamhitaji basi ni wakati mwafaka wa kumfuata na kumweleza
ukweli na kirahisi nakuhakikishia unabeba mzigo kwani ni mtu tayari
aliyekuwa anahisia kali za mahaba juu yako.