Kituo cha uhamiaji kati ya mpaka wa Cameroon na Nigeria
Makasisi wawili kutoka nchini
Italy pamoja na mwanamke mmoja raia wa Canada waliotekwanyara na kundi
la Boko Haram nchini Cameroon wameachiliwa huru.
Idara ya mawasiliano nchini Cameroon imesema
watatu hao wako katika afya nzuri na wameabiri ndege inayoelekea katika
mji mkuu wa Younde.
Walipelekwa kasikazini mwa taifa hilo karibu na mpaka na Nigeria.
Majina ya makasisi hao ni Giampaolo Martana na Giantonio Allegri.