Timu
ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imetoka sare ya bao 2-2 na timu ya
Taifa ya Zimbabwe kwenye mchezo ulipigwa Uwanja wa Taifa jijini Harare.
Mechi hiyo ilikuwa ni ya marudiano ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Africa zitakazopigwa mwakani nchini Morocco.
Katika mchezo huo magoli ya Stars yamefungwa na Nadir Haroub 'Cannavaro' dakika ya 21ya kipindi cha kwanza huku la pili likifungwa na Thomas Ulimwengu dakika ya 46.
Magoli ya Zimbabwe yamefungwa na Phiri katika 10 wakati la pili likiwekwa kwenye kamba na Katsande dakika ya 55.
Hivyo Stars imesonga mbele kwa
jumla ya mabao 3-2 na inasubiri makundi sasa.
Timu nyingine za Afirka Mashariki
zimesonga mbele ambazo ni Kenya, Uganda na Rwanda ambayo iliitungua Libya magoli 3-0.