Mama Mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kasikazini Mh.Zitto Kabwe, Bi.Shida Salum amefariki dunia leo katika hospitali ya AMI ya jijini Dar Es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Mh. Zitto Kabwe mwenye kanzu nyeusi akiwa na Prof. Ibrahim Lipumba, wakiuaga mwili wa marehemu mama yake Zitto Kabwe, Bi.Shida Salum kabla ya kusafirishwa kigoma kwa mazishi.
Waheshimiwa
Wabunge na Baadhi ya Viongozi wakibeba Jeneza lililobeba Mwili wa
Marehemu Mama Yake Zitto Kabwe Bi. Shida Salum wakiuingiza kwenye ndege
Tayari kwa safari ya kwenda Kigoma Kwa mazishi.
Ndege iliyobeba mwili wa marehemu mama yake Zitto Kabwe, ikiandaliwa kwa ajili ya safari ya kuelekea Kigoma kwa ajili ya shughuli ya mazishi
Prof. Ibrahim Lipumba akishauriana jambo baada ya kuupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea Kigoma.
Rais wa Taswa Juma pinto (kushoto) akiwa na Muadhama Polycarp Cardinal Pengo walipokutana Termina1 v.i.p Airport wakati wa kuuaga mwili wa marehemu mama yake Zitto Kabwe.
Mama yake mzazi Zitto Kabwe Marehemu Bi. Asha Salum enzi za uhai wake.