NEWS UPDATES: Jumla ya watu. 12 wamepoteza Maisha na 22 wamejeruhiwa leo baada ya
basi la New Force kupata ajali Eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani
Iringa barabara kuu ya Iringa- Dar es salaam..

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,Peter Kakamba amethibitisha watu 12 kupoteza maisha
katika ajali hiyo. Wanane ni wanae na wanne ni wanawake. Abiria 28
wamejeruhiwa wakiwemo madereva wa basi la lori na hali zao siyo nzuri.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane alasiri ambapo basi la kampuni
ya Newforce aina ya Youtong lenye namba za usajili T483CTF likitoka
Tunduma kwenda Dar limegongana na lori aina ya Scania lenye namba
T616DEF katika kijiji cha Mahenge,wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa katika
barabara kuu ya Dar - Mbeya.
Sehemu ya basi la New Force One baada ya kupata ajali
Majeruhi wamelazwa hospitali ya wilaya ya Ilula.kilomita 45 kutoka Iringa mjini. kadhaa wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine wengi wakijeruhiwa baada
ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya Kampuni ya NEW FORCE ONE lenye
namba za usajili T483 CTF kupinduka mapema mchana wa leo katika eneo la
Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa- Morogoro,
jitihada za kusafirisha majeruhi zinaendelea.

Chanzocha ajali hiyo, inaelezwa kuwa ni Lori la mizigo lililokuwa likitokea
upande wa Morogoro, kupasuka tairi ya mbele na kupoteza muelekeo
uliopelekea kuligonga basi hilo na kupinduka. Globu ya Jamii inafanya
jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa kwa taarifa zaidi.
tutaendelea kuwaletea taarifa kadri tutakavyozipata.
Ajari mbaya sana imetokea muda huu maeneo ya kitonga na mikumi watu 12 wamepoteza maisha .mungu awapumzishe kwa amani