Mh. MANSOUR YUSSUF HIMID
Chama cha
wananchi CUF kimetoa msimamo wake wakuto hudhuria kwenye sherehe za
Mapinduzi kwa walichodai kuwa hawatambui uongozi uliopo madarakani
visiwani humo.
Msimamo huo mzito umetolewa na mshauri mkuu wa katibu mkuu
wa chama hicho Mhe Mansour Yussuf Himid kwa niaba ya Maalim Seif ambaye
pia ni makamu wa kwanza wa rais ambapo amesema CUF kinaamini kuwa
uongozi uliokuwepo sasa si uongozi uliotokana na nguvu za wanananchi
huku akisema sherehe hizo huwa zinaongozwa na rais aliyechaguliwa
kikatiba na siyo ambaye muda wake na uuongozi mzima umemaliza muda wao.
Kiongzoi
huyo wa CUF ambaye amewahi kuwa mshika fedha wa CCM Zanzibar na waziri
katika awamu mbili za Amani Akrume na awamu ya Dr.Shein kabla kutimuliwa
ndani ya CCM amemsmea malengo ya mapinduzi ya waasisi wake yalikuwa ni
kuwa na nchi ianyongozwa na ridhaa za wananchi hivyo CUF imeamua kususia
sherehe hizo hadi sheria na katiba ya nchi itap[oheshimiwa.
sherehe
za mapinduzi zinatarajiwa kuanza januari mbili huku kwa mujibu ya ratiba
ya sherehe hizo zinaonyesha kuwa maalim seif na viongozi wa CUF
wakiwemio mawaziri wa cuf wameshirikishwa katika uiznduzi wa miradi
mbali mbali ya sherehe hizo za kutimiza miaka 52 ya mapinduiz ya
zanzibari.